Sunday, April 5, 2009

KAMANDA KOVA:TUTAMNASA DEREVA WA BAJAJI!


Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova, amesema jeshi lake litahakikisha linamtia nguvuni dereva wa bajaji iliyogongana na gari alilokuwa akiliendesha Mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge. Kova alisema hayo jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa tathmini kuhusu matukio yaliyojitokeza katika wiki nzima jijini.
Alisema baada ya mmiliki wa Bajaj hiyo, Majid Gharib(26) kujitokeza juzi, jeshi lake linaendeleza juhudi za kumsaka dereva wake aliyetambulika kwa jina la Abdallah Hamisi.
"Jeshi la Polisi halishindwi kitu na tupo hapa kwa kazi moja ya kukamata wahalifu na wote wanaoharibu sheria zetu za nchi, hivyo dereva huyo huyo tutamtia nguvuni muda si mrefu hilo naahidi" alisema Kova kwa kusisitiza.
Mmilikiwa bajaj iliyosababisha vifo vya wanawake wawili, Vicky na Beatrice Contanstine, Mbunge Chenge alikuwa na gari aina ya Toyota Hilux yenye namba T 512ACE ambayo akiwa dereva mwenyewe aligonga Bajaj yenye namba T736 AXC na dereva wa Bajaj hiyo kutoweka kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker