Thursday, April 16, 2009

Mambo si Salama kwa Waendesha Baiskeli Bongo!

Hivi sasa katika njia mbali mbali za jiji la Dar es salaam, imekuwa si salama kwa waendesha pikipiki na hata baiskeli kutokana na wimbi la uporaji kufuatia vibaka kuwakaba na kuwajeruhi waendeshao vyombo hivyo na kisha kupotea navyo.
Pichani ni mmoja wa waathirika wa tukio kama hilo. Anaitwa Katundu Chema(40) mkazi wa Kigogo Mbuyuni. Anasema kwamba alikuwa anarudi nyumbani akitoka kibaruani, akaamua kupitia barabara ya Kawawa kuelekea Kigogo ndipo alipofika katika bonde mbele kidogo ya Travertine Hotel ndipo akavamiwa na vijana wapatao wanne, wakamkata kwa mapanga kichwani na kisha kuchukua kila walichokiona pamoja na baiskeli yake.Majeraha yaliathiri sehemu ya ubongo na hivyo kupelekea yeye kutoweza kuongea kabisa. Sasa hivi ameanza kujitahidi kuongea kama mtoto mdogo.Picha inaonyesha jeraha la kichwani.
Katundu anasema kwa masikitiko "Unajua, nilikuwa fundi seremala kwa muda mrefu mkoani morogoro ndiyo nikaja Dar es salaam kutafuta maisha. Nilifanya useremala kwa kujiajiri mpaka juzi juzi ndiyo nilipata kazi kampuni ya NPK Technologies kama fundi wa kutengeneza vitasa vya kisasa vya kutumia kadi za elektroniki au alama za vidole. Nilifanya kazi kwa siku 5 tu, ndipo nikapata mkasa. Hali hii inanisumbua sana, sijui ndio nimeshakuwa kilema?Sijui kazi nitaweza tena? Sijui kama nitarudishwa kazini?"
Hayo yote ni maswali ambayo Katundu anajiuliza,na inavyoonekana ni kwamba bado anaumwa na anahitaji matibabu zaidi.


No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker