Tuesday, April 14, 2009

Ajali za Easter.......Watoto Kutoka Coco Beach Wapata Ajali!!

Kabla ya kuanza kwa Sikukuu ya Pasaka, nilitoa tahadhari juu ya uendeshaji wa magari ili kuepuka ajali. Lakini kutokana na ajali zilizojitokeza katika kipindi hicho inaonekana kwamba mambo hayakuwa hivyo. Mbali na ripoti niliyotoa jana za ajali kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili(MOI), leo Afisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi, amesema kwamba jana usiku ilitokea ajali nyingine ya kusikitisha ambapo watoto waliokuwa wanatoka Coco Beach kusherehekea Pasaka, walipata ajali kutokana na gari waliyokuwemo aina ya Hiace Kuendeshwa kwa Mwendo kasi.
Habari za kipolisi zinasema kwamba, ajali ilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku barabara ya Haille Selasie katika eneo la St. Peters Oysterbay. imeripotiwa kwamba, gari yenye namba za usajili T 127 AGY iliyokuwa ikienda kasi na dereva alishindwa kuhimili gari na kuacha njia na kupinduka. Watoto 7 walijeruhiwa, watano waliruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya mwananyamala. Watoto wawili walipewa rufaa kwenda MOI kutokana na kwamba hali zao kuwa mbaya sana. Hao ni Moses Kilian(14) darasa la 7 shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga. Ameumia kifuani, usoni na kichwani. Mtoto mwingine ni Aziz Selemani(7) anayesema darasa na shule hiyohiyo aliyopo Moses, ambaye amevunjika mkono.

Hali ya Moses bado ni tata japo madaktari wanafanya kila jitihada kumsaidia.

Dereva wa Hiace ametoroka na hajulikani alipo baada ya ajali.

yES! Tunawatakia ahueni ya haraka vijana wote waliopata ajali .

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker