Wednesday, April 22, 2009

Kibano kwa Dereva wa Bajaji!

Mambo si mazuri sana kwa madereva wa bajaji na pikipiki.Pichani wanaonekana askari wa kikosi maalum cha kudhibiti uhalifu ambao  jijini Dar es salaam hujulikana sana kama "voda fasta" au Tigo wakiwadhiti madereva wa bajaji na pikipiki, ikiwa ni jitihada za kudhibiti ajali zitokanazo na vyombo hivyo vya usafiri.
Nafikiri kinachotakiwa ni kuwaelimisha madereva hawa wajibu wao, baada ya hapo wakikaidi maagizo watakayopewa ndio adhabu ifuate.Inaonekana wengi wao wamekurupuka tu katika biashara hiyo bila kujua ni nini wanachotakiwa kufanya au kufuata. Tanzania sio nchi pekee au nchi ya kwanza kutumia usafiri wa aina hiyo. Lakini hawana kiwango cha ajali cha kutisha kama ilivyo hapa nchini kwa sasa.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya mifupa na Ajali(MOI), wanapokea sio chini ya wagonjwa watano wa ajali zinazotokana na vyombo hivyo. ni muhimu kujua kwanza tatizo li wapi, ndio ufumbuzi utafutwe (Picha ya Guardian).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker