Wednesday, April 1, 2009

He! Nini tena?

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa usalama barabarani wametoa tamko lililowashtua wengi kwamba Leo hawatafanya kazi ya kuongoza magari siku nzima! Tamko hili limeshtua watumiaji wengi wa barabara za jiji ,kwa kujua kwamba hali italifanya jiji lisimame kwani msongamano wa magari utakuwa si wa kawaida.
Mpaka muda huu barabara zote za jiji hazipitiki, shughuli zimesimama na wananchi wameamua kutembea kwa miguu kutoka kila kona ya jiji. Kamanda Suleiman Kova alipopigiwa simu ili kujua kama huu ni mgomo au la, amesema hana la kuzungumza kwa sasa na anaendelea kufuatilia kujua chanzo cha hilo na taarifa zaidi atatoa katika kikao chake na waandishi wa habari leo saa 4 kamili asubuhi hii.
Kwa ushauri, wale ambao hawajatoka majumbani ni vema wakilala na kusubiri tamko la Kamanda kova kwani huko barabarani hakupitiki kamwe!(hey, what is the date today?Just relax!)

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker