Monday, April 6, 2009

Ajali za Pikipiki Zaongezeka Moro!


Ajali za pikipiki katika Manispaa ya Morogoro, zinazidi kuongezeka, yakiwa ni matokeo ya waendesha pikipiki hizo kuanza tena kuvunja sheria za barabarani.Pamoja na mambo mengine, waendesha piukipiki wamefufua upya mtindo wa kubeba abiria zaidi ya mmoja, maarufu kama mshkaki, katika kila pikipiki.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Morogoro, Ibrahim Mwamakula,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.mwamakula alisema ajali zinazotokana na matumizi mabaya ya pikipiki zimeongezeka katika siku za karibuni. Alisema hali hiyo inatokana na waendeshaji wa vyombo hivyo, kujisahau na kuanza tena kuvunja sheria ya usalama barabarani.

Alisema kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hilo, askari wa usalama barabarani, wanakusudia kuendesha operesheni ya kuzikamata pikipiki zisizosajiliwa na madereva wasio na leseni(picha kutoka katika mtandao).

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker