Friday, April 10, 2009

Pikipiki Nazo, Mh!.......Kaazi Kweli kweli!
Arnold Aaron (30) amelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na ajali kufuatia ajali ya pikipiki. Alipata ajali akiwa anatoka Mwenge kwenda Mbezi. Anasema alipofika njia Panda ya Mbuyuni alikodi pikipiki ili imfikishe nyumbani kwake ambako ni Km 1 kutoka Bagamoyo Road. Anasema ilitokea gari ikawapita(overtake) na ghafla ikasimama na kuanza kurudi kinyumenyume(reverse) na kuigonga pikipiki yao. Kufuatia tukio hilo, alipata maumivu ya kichwa(Head injury).
Mussa Aluwa(51) mkazi wa Chanika anasema kwamba alipata ajali akiwa anatoka nyumbani kwake kuelekea dukani kuchaji simu yake yapata majira ya saa 1 usiku, ndipo pikipiki ambayo ilikuwa haina taa ikakata kona ya ghafla na kumgonga. Anasema baada ya kugongwa alipoteza fahamu siku ya pili ndio alishtuka kujikuta yupo katika wodi ya MOI. Musaa alivunjika mguu sehemu ya paja na kupata michubuko sehemu zote za mwili.
Mohamed Ally Mbwana(37) anasema kwamba alipaki pikipiki alipokuwa anajiandaa kushuka, akasahau kwamba switch ilikuwa ‘on’ na akawa ameachia clutch, ndipo pikipiki ikaruka juu na kumdondokea mguuni na kumvunja mguu chini ya goti.Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa MOI Bwana Jumaa Almasi,wagonjwa wote hao wanaendelea vema na hali zao zinaridhisha.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker