Mbunge wa Biharamulo kwa chama cha TLP Phares Kabuye pamoja na watu wengine wawili wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magubike wilayani Kilosa jana saa 1 asubuhi.
Gari lililopata ajali lina namba za usajili T 934 ADA la kampuni ya RS Investment kama
linavyoonekana pichani.Lilikuwa likitoka Bukoba kuelekea Dar es salaam.
Inasemekana kwamba dereva wa basi alimpa "deiwaka" kondakta wake ambapo lilimshinda na kuacha njia akiwa katika mwendo wa kasi na hatimaye kupinduka. Kondakta na dereva wake hawajulikani walipo baada ya kukimbia (Picha:Bunge na Habari Leo na Bunge).
yES! Kilio changu kipo pale pale, tuungane kutokomeza jinamizi la ajali.
I like your blog.
ReplyDeleteThanx for visiting Dyanna,ur most welcome. I gonna visit your blog and learn something new from you.
ReplyDeleteMkuu hizi ajali sidhani kama zitakuja kuisha kama hakuna ushirikiano wa kutosha kutoka kwa ndugu zetu wa usalama barabarani.Basi linatoka Bukoba kuja Dar lina dereve mmoja!Trafiki wanaangalia tu likipita!Nchi yetu tunaiangamiza wenyewe kwa kupenda njia za mkato, huku maisha ya wenzetu yakiteketea kila kukicha!
ReplyDeleteNi kweli mzee, yani ukiona ajali zinavyoingia hapo MOI kwa siku, hali inatisha. Jana nilitembelea MOI ndio nikapata hizo ajali nilizoripoti.Naahidi kupita huko kesho ili nichanganye za leo na kesho, utashangaa jinsi idadi ilivyo kubwa.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe kwamba, askari wa usalama barabarani wana wajibu mkubwa sana kukabiliana na tatizo hili, lakini hawatekelezi wajibu wao. Kila kukicha tunapoteza watu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa hili.
Kwa mfano, Bajaji ni usafiri unaotumika miaka nenda rudi katika nchi za mashariki ya mbali. Jana nilikuwa naongea na mtanzania anayeishi huko, ameonyesha kushtushwa na ajali za Bajaji hapa nchini na anajiuliza kwanini sisi?Jiji la Mombasa linatumia Bajaji kwa kiwango kikubwa sana, lakini kwa kipindi nilichopata nafasi ya kukaa huko, sijashuhudia ajali ya Bajaji hata moja.
sasa tujiulize, ni wapi hapajakamilika?