Saturday, April 11, 2009

Kova Afichua Siri ya Mabasi Kutekwa Mikoani!

Polisi Kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam, imesema utekaji wa magari unaofanywa na majambazi maeneo ya mikoani, kwa kiasi kikubwa unasabababishwa na usafirishaji kwa kutumia mabasi.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova alisema jana utekaji wa mabasi umeongezeka kwa sababu wafanyabiashara wenzao wa jijini Dar es salaam.

"Wafanyakazi wengi wa mikoani, wanatumia mabasi ya abiria kutuma fedha kwa wafanyabiashara wenzao wa Dar es salaam, hili linachochea vitendo vya kutekwa kwa mabasi kwa sababu taarifaa za usafirishaji zinavuja", alisema Kova.

Kwa mujibu wa Kova, wafanyabiashara hao, wamekuwa wakinunua fedha za nchi mbalimbali na kuzisafirisha kwenda Dar es salaam ambako zinauzwa na kupata fedha nyingi za kitanzania.

"Ni biashara nzuri wengi hununua fedha za nchi jirani na kisha kusafirisha kwenda jijini Dar es salaam kwa lengo la kuzibadilisha na kuwa katika fedha za kitanzania, wanapata faida zaidi", alisema Kova.

Alisema biashara hiyo ni nzuri lakini ni hatari kwa usalama wa maisha ya wanaojihusisha nayo.

Kamanda Kova alisema tatizo linalowafanya wafanyabiashara hao kusafirisha fedha zao kwa kutumia magari linatokana na kukataliwa kwa fedha za kigeni katika mabenki ya kitanzania.

"Nimeongea nao wamenieleza matatizo yao kuwa ni benki zinakataa fedha za kigeni lakini baada ya kuongea na wakurugenzi wa benki hizo, wamekubaliana kupokea fedha za kigeni, ili kurahisisha usafirishaji na kuepusha ujambazi wa kuteka magari mara kwa mara" alisema Kova.

Kova alisema tatizo kama hilo limejitokeza maeneo ya Tunduma mkoani Mbeya, ambako wengi wamesema walikataliwa kutumia benki kwa ajili ya kutuma fedha zao kigeni, kwa lengo la kuziuza jijini Dar es salaam (Mwananchi).

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker