Wednesday, April 15, 2009

Zebra Crossing, Je Watembea kwa miguu Wanajua Wajibu Wao?

Kwa miaka mingi tokea nikiwa mtumiaji wa barabara, nimejifunza alama mbalimbali zikiwamo zebra crossings!

Kwa kawaida Zebra crossing au Kivuko cha watembea kwa miguu, ni eneo ambalo magari yanapaswa kusimama na kuwaachia watembea kwa miguu wavuke. Katika miaka yote hiyo, nimejifunza kitu kimoja kwamba,si watembea kwa miguu wala madereva ambao wanajua wajibu wao.

Katika zunguka zunguka yangu hasa hasa katika barabara za Dar es salaam, ni mara chache sana madereva wanaheshimu zebra crossing na kusimama. Kila dereva anaonekana kuwa na haraka na mara nyingine hutishia hata kuwagonga watumiaji wengine wa barabara. Kwa upane wa daladala, wao hujifanya wamesimama kumbe wanapakia abiria!

Tukija kwa watembea kwa miguu,nimeona mara zote ninapofika katika eneo hilo kwamba, wanapoachiwa kuvuka, basi huvuka kwa kutembea kama konokono. Wanakuwa hawana haraka kabisa,jambo ambalo huwafanya baadhi ya madereva ambao si wastaarabu kutishia kama wanaondoa gari!

Tatizo jingine ni kwamba,pamoja na kwamba hilo ni eneo la kuvuka, ni lazima pia kabla mtu hajaamua kuvuka aangalie gari linakuja kwa kasi gani. Mara nyingine nimeona watu wanakaribia kugongwa kwa sababu wanatoka upande wa pili wa barabara na kukimbia hadi upande mwingine wa barabra bila kuangalia kasi ya gari inayokuja.

Nafikiri bado wananchi wengi hawajaelimika juu ya matumizi ya zebra crossing hivyo elimu zaidi inahitajika.

Kwa upande wa TANROADS, nafikiri wana wajibu wa kuzichora hizi alama ili zionekane vizuri zaidi. Pichani ni zebra crossing iliyopo manzese ambayo imefutika kabisa.Nawasilisha.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker