Thursday, April 16, 2009

Hii ndiyo Bongo Bwana!Picha hizi zinaonyesha hali ilivyokuwa yapata wiki tatu zilizopita, baada ya mvua kubwa kunyesha Dar es salaam. Na inakuwa hivyo mara zote mvua ikinyesha Dar. Inaonekana watanzania tunasahau haraka sana. Siku mvua iliponyesha kila mtu alilalamikia miundo mbinu mibovu na kwamba jitihada zifanyike kutatua tatizo hili. Baada ya mvua? kimyaaaa! Tunasubiri mvua nyingine kubwa ikiwa kama hivyo ndio tuanze tena makelele.Ndiyo nayaita makele, kwa sababu hakuna anayeonyesha kujali.
Nafikiri mamlaka husika, kama ni DAWASA au TANROADS au zote kwa pamoja, zichukue hatua za kurekebisha hali hiyo kwani watu hupata usumbufu na kupoteza mali au mali zao kuharibika.(Picha kutoka Bongo Pix blog).


No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker