Tuesday, April 14, 2009

Pikipiki Tena..!Hit and Run!

Leo asubuhi saa 12.15 imetokea ajali mbaya sana eneo la Bahama Mama(Kimara)ambapo mwendesha pikipiki amegongwa na gari na kuumia vibaya sana. Akiwa anagaagaa kwa maumivu na kutapakaa damu mwili mzima alionekana kuwa ameumia zaidi kichwa kwani alionekana kutokuwa na fahamu.
Gari iliyomgonga haikujulikana lakini alikuwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajili T545AVA. Baada ya kutopata msaada kwa muda, alitokea msamaria mwema mwenye gari namba T820 ANK ambaye alimchukua na kumpa msaada wa kwenda hospitali.
Kwa mara nyingine nilisikitika kuona kwamba aliyegonga kakimbia, na waliokuwepo katika eneo la tukio walikuwa wanamshangaa majeruhi badala ya kutoa msaada.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker