Friday, April 3, 2009

Taa za Barabarani Zinabaki Milingoti tu?


Ni lini tutakuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba taa za barabarani(street lights) zinatunzwa na kuendelea kufanya kazi miaka kadhaa tangu zilipowekwa? Nauliza hivyo kwa sababu taa nyingi katika barabara zetu mpya hufanya kazi vizuri kabla ya barabara kukabidhiwa kwa serikali. Inapotokea barabara inakabidhiwa tu nazo huacha kufanya kazi. Nina mifano kadhaa. Kwa mfano taa za Morogoro Road kuanzia Ubungo hadi Kimara Resort zimebaki ni mapambo ya milingoti kwa sababu nyingi(asilimia 90%) hazifanyi kazi. Na barabara ya Sam Nujoma nayo ni vivyo hivyo, japo hii haina hata siku nyingi.

Ninaamini mbali na kupendezesha jiji(kama inavyoonekana katika eneo la Sinza kutokea Mori baada ya kuwekwa (street lights )pia zinasaidia kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa.

Kama inavyoonekana pichani, kuna kitengo maalum cha Umeme cha Tanroads lakini sioni kama jitihada zao zinatosha.

Kutokana na ongezeko la vibaka, nafikiri ni muhimu kama hizi taa zitafanyiwa kazi na kuhakikisha kwamba zinawaka kama inavyotarajiwa (Photo by The Daily News).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker