Thursday, April 16, 2009

Hii Tena imezidi! No number Plate! Pt. 2

Gari la kubeba takataka (juu katikati) linaonekana likipita bila namba ya usajili .
Bado tunaendelea kuyatupia macho magari ya kubebea takataka. Mara ya mwisho tuliona kwamba mengi yana mapungufu na mengine hayana namba usajili kabisa, lakini yanatembea barabarani na mengi yamekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara. Cha kusikitisha ni kwamba, yanapita katika barabara zetu na vyombo vya usalama vinayaona na kuyafumbia macho. Yakishaleta madhara ndio tutaona kila mmoja anazinduka usingizini na kuanza kuyafuatilia. kwanini yasifuatiliwe sasa?

Magari ya takataka ambayo hayana namba za usaji kama hilo hapo juu pichani,yanaendelea kudunda katika mitaa ya jiji la Dar. Je, nani wa kumuuliza kuhusu hilo?

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker