Sunday, April 19, 2009

Waendesha Magari Wengi Madereva Wachache!


Ndiyo!waendesha magari wengi madereva wachache kwa maana ya kwamba, udereva ni fani na inahitaji ujuzi ili kuifanya kwa ufanisi. Mtu yeyote anaweza akakaa nyuma ya usukani wa gari na kuliendesha.
Nasema hivyo kwa maana ya kwamba, ni madereva wachache sana ambao wanajua hata jinsi ya kutumia taa zao wakati wa usiku. Nimeleta picha hii ili muweze kupata picha , hapa ni barabara ya Morogoro kigiza ndio kwanza kinaanza, angalia gari inayokuja upande wa pili wa barabara, amewasha taa kubwa 'full light' kama vile yupo porini kiasi cha kuwafanya madereva wengine washindwe kuona. Na watu kama hawa hata ukimpa ishara ya kuzima hizo taa na awashe za kawaida hata hajui. Wa namna hiyo si 'dereva' bali ni 'mwendesha gari'. majadala uko wazi!

3 comments:

  1. Umenena Tram!Dar ina waongoza magari tena hata bora waendesha magari..mtu anajua kukanyaga mafuta,kufunga breki,kubadili auto- gear ili gari itembee na kuzungusha sterling tu!taa, anajua kuziwasha full tu muda wote. Huyo ndiye utakuta hata gari ikiharibika hajui ai-park namna gani na awashe hazard lights na kuweka triangle signs au alama nyingine ya tahadhari!Ajali nyingi zinasababishwa na hizi leseni za kuletewa nyumbani! Sijui lini hali hii itakwisha!

    ReplyDelete
  2. Nashukuru wadau kama wewe kuliona hilo, maana tutakuwa tunaimba nyimbo za "ajali ajali" kila kukicha.Lakini hakuna mabadiliko.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli MR. BOBOS! kabisa Dar inaongoza kwa kutokuwa na madereva bali 'waendesha magari' maana mtu akipata mkopo wa 'SACCOS' anataka nae atoke vipi na 'SACCOS CAR' yake, hapo ndo utaona nani dereva na nani mfukuza upepo barabarani. Ujumbe kwa wadau 'wazee wa feva'(Polisi wa usalama barabarani tuokoeni na hili jinamizi la ajali maana litatumaliza na kusababisha nguvu kazi kupungua na kutuletea yatima wengi nchini mwetu

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker