Monday, April 20, 2009

MAGARI MADOGO HATARI-Utafiti!

"Yana bei nafuu, yanatumia mafuta kidogo. Lakini usalama wake katika ajali ni mdogo"
WASHINGTON, MAREKANI:Wanaomiliki magari madogo wanaweza kuwa wananufaika na utumiaji mdogo wa mafuta na pia unafuu wa bei za vyombo hivyo vya usafiri, lakini sekta ya bima inasema yanaongoz akwa kugongana na magari makubwa.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa ajali yaliyotolewa jana, Taasisi ya Bima ya Usalama wa barabara Kuu ilibaini kuwa madereva wa magari yaliyotolewa mwaka 2009 ya smart ''for two'', ''Honda fit'' na ''Toyota Yaris'' wanaweza kupata majeraha ya miguuni na kichwani kutokana na gari hizo kugongana na malori au magari ya saizi ya kati.
''Kuna sababu nzuri za watu kununua gari ndogo. Yana bei nafuu yanatumia mafuta kidogo. Lakini usalama wake katika ajali ni mdogo'' alisema Adrian Lund, Rais wa Taasisi hiyo.
Watengenezaji wa magari madogo walisema utafiti huo ulitokana na ajali zilizosababishwa na uendeshaji wa kasi ambazo hutokea kwa nadra sana barabarani. Pia walisema utafiti huo umerejesha hoja ya zamani ya sekta ya bima dhidi ya haja ya kuwa na magari ambayo yanatumia mafuta vizuri......(habari zaidi, Mwananchi, 20 April, 2009).

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker