Mustafa Mboweto(29) mkazi wa Goba amefikishwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili (MOI) leo baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu wa kushoto katika kifundo cha mguu (ankle joint).Amesema yeye alikuwa 'deiwaka' katika lori la mchanga ambapo lilifika njiano kukuta lori la kuuza maji likiwa limepaki kando ya barabara, wakati wakijiandaa kulipita lori hilo ghafla dereva aliliingiza barabarani.Kwa kuwa yeye na mwenzake walikuwa wameshuka ili kumuelekeza dereva wao jinsi kulipita lori hilo,dereva wa lori lao alipokuwa anakwepa aliwafuata na yeye kukanyagwa mguu.
Pichani ni Macdizel Kwimba(28) ambaye pia alifikishwa MOI baada ya mashine kumkatakata mkono na hatimaye mkono ukakatwa baada ya kuwa katika hali mbaya sana. Anasema anafanya kiwanda cha COTEX Mbezi Beach. Anasema alipokuwa akiendesha mashine ndipo mkono ukavutwa na 'kutafunwa' na mashine. Jana alipokelewa mgonjwa mwingine kutoka COTEX,Habiba Abdallah(29)mkazi wa Kunduchi Mtongani, ambaye alikatwa vidole na feni ya machine.Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa MOI amethibitisha kuwapokea majeruhi hao na amesema kwamba mara kwa mara wamekuwa wakipokea majeruhi wa kutoka COTEX wakiwa wameumia au kukatika mikono.
Wakati huo huo, Afisa Uhusiano wa MOI ametoa taarifa kwamba, Mkufunzi wa Chuo cha Zima Moto na Uokoaji, Bwana Marwa Mashana(37) amepokelewa hospitali hapo baada ya kupata ajali akiwa anaelekea Sokoine Morogoro. kufuatia ajali hiyo, ameumia mgongo(uliosababisha asiweze kuhisi kuanzia kiunoni hadi miguuni),mkono na kichwa.
wengine waliopokelewa leo ni Kulwa Hamisi(33)ambaye ameumia kichwa baada ya kugongwa na gari akiwa mtembea kwa miguu. E7758 PC Charles Emmanuel(36) mkazi wa Mtoni kijichi ambaye amevunjika mguu sehemu ya paja baada ya kupata ajali akiwa abiria wa Bajaji. Juma Musa(adult) wa kutoka Kibada, naye amepokelewa MOI akiwa amevunjika mguu sehemu ya paja, amegongwa na gari akiwa mtembea kwa miguu.
Kwa Mujibu wa Jumaa, wote wanaendelea vema.
No comments:
Post a Comment