Thursday, April 30, 2009

DAR STUDENTS TRANSPORTATION!





Hali hii mpaka lini?

Mabomu Yajeruhi na Kuua!(Explosions at Armoury)

Watu walipochanganyikiwa na milipuko ya mabomu


Wauguzi wa hospitali ya Temeke wakiwashusha majeruhi MOI

Majeruhi akiwa chini ya uangalizi wa madaktari


Mmoja wa majeruhi aliumia kama hivi,na mwingine alipoteza mguu kabisa
Mtoto wa miaka saba ambaye hakutambulika jina lake hadi leo alipoweza kuongea na kusema kwamba anaitwa Khadija Zomboko. Anasema watu walipokuwa wanakimbia, walimkanyaga na kumvunja mkono!


Madaktari na maafisa wa MOI wakijaribu kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa watoto waliofikishwa hapo.

Gari za wagonjwa kutoka kila kona ya Dar zilibeba majeruhi

Majeruhi wakishushwa MOI, palikuwa hapatoshi!


Wauguzi wa MOI wakimpatia msaada mmoja wa majeruhi



Kibaka chini ya ulinzi, "ati kufa kufaana, leo utashaa!"

Kibaka aliyejaribu kuiba wakati wa milipuko mbaroni


Masalia ya bomu lililolipuka

Moja ya nyumba zilizoathirika
Moshi mzito baada ya bomu kulipuka
Kaazi kweli kweli, wingu zito!
Wingu na moto! (Picha na Hamisi Bilali)

Kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali(MOI) taarifa inasema kwamba majeruhi waliofikishwa hapo ni 26,kati ya hao, wawili wamelazwa ICU, 14 wamelazwa,9 walipata matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani na mmoja alipata matibabu na kupelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa alikuwa ni mja mzito, hivyo ataonana na madaktari bingwa wa kinamama.


Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano mwandamizi wa MOI Bw. Jumaa Almasi, walioumia sana ni Zulfa Hamisi ambaye amekatika mguu kutokana na mlipuko na Juma Sobo ambaye aliumia kichwani na kupoteza meno kadhaa.


Wakati huohuo, Rais wa Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, William Lukuvi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Waziri wa Afya Prof Mwakyusa,ametembelea MOI na kuwapa pole majeruhi waliolazwa katika Taasisi hiyo.


Kiongozi mwingine wa kitaifa aliyefika MOI ni Makamu wa Rais, Dr. Ali Mohamed Shein aliyefika kuwapa pole majeruhi pia.
(Rais Kikwete akiwa MOI ICU. Source: Michuzi Blog)



(More than 100 people have been injured following explosions at Dar es salaam Armoury. The bomb exploded from fourr out of 11 armouries at the camp of the Pople's Defence Force (TPDF) caused panic and paralysed activities for the whole day).

Tuesday, April 28, 2009

USO KWA USO!

Same make, Same models zinapogongana!



The Road was clear, but there was this accident! ama kweli, ajali haijalishi mazingira!



Monday, April 27, 2009

Agongwa na Bajaji

Anayeonekana pichani ni Bwana Mwarami akisimulia jinsi alivyogongwa na Bajaj akiwa pembeni ya barabara na kuvunjika mfupa wa goti(patella).Anasema ni kutokana na uendeshaji mbaya wa Bajaj uliopelekea yeye kugongwa.

Jingine Tena..........No numbers!

Hapa linaonekana likiweka mafuta bila wasiwasi

Hapa linaanza kukata mitaa kwa nafasi!

Huu ni muendelezo wa ufuatiliaji wa haya magari ya takataka ambayo yanaonekana kukatiza mitaa ya jiji bila hata namba za usajili. Sijui wahusika wanayaona au vipi. Nimekuwa nikifuatilia na nitaendelea kufuatilia mpaka hapo wahusika watakapoona umuhimu wa kuyafuatilia.






Sunday, April 26, 2009

Hatari Kwa Kijana Huyu!

Kijana unayemuona nyuma ya lori linaloonekana pichani, ni mlemavu ambaye amepoteza miguu yote, haijulikani ni kwa ajali au kwanini.Amejifunza kutembea kwa kutumia magoti, kwani inaonekana miguu ilikatwa chini kidogo ya goti. Mara nyingi anapatikana maeneo ya taa za kuongozea magari za Magomeni aidha kwa upande wa Barabara ya Kawawa au Morogoro.Anachofanya hapo huomba msaada wa pesa katika magari yanayopita njia hizo.
Ninachotaka kuongelea hapa ni hatari ya kijana huyo kugongwa na gari kwani wakati mwingine hukaa katikati ya barabara.
 Si magari yote yana breki nzuri au hata kama gari lina breki nzuri, zinaweza kuleta matatizo na hivyo kupelekea yeye kugongwa.
Leo Dar es salaam kulikuwa na mvua kubwa, nimemkuta maeneo hayo hayo. Kipindi cha mvua magari mengi huwa na matatizo ya breki,na pia magari huserereka yanapofunga breki.Je hiyo si hatari kwake? Je,askari wa usalama barabarani hawana jukumu la kumuelimisha huyu kijana?Mara nyingi anakuwa karibu na askari muongoza magari iwe asubuhi au jioni au hawamuoni? siamini hivyo!
Kuna haja ya kumuepusha huyu kijana na hatari hii, kwani naona hatari inayomkabili mbeleni.

What is Trauma?

Many of my readers wanted to ''why Trauma Class'' or rather ''What is this Trauma am refering to?''Here is the clarification according to google definition:

The word "Trauma" refers to a wound or an injury, whether psychic or physical. The word is also synonymous with the word accident, referring to an unexpected, unforeseen and unfortunate event. Disability or death from injury is viewed as an act of God or an unpreventable accident. It is true that no one expects to be injured; however in most of the cases, "accidents" are preventable. All that is required is a small amount of planning.
Now you know, this is not only a blog but also a class about trauma, the effects of trauma, suggestions and opinion about trauma etc. Karibu.

Ujumbe Kwa TANROADS! Jangwani Area!

Kaazi kweli kweli!
Hapo jee?
Niingie nisiingie?Wenye magari madogo wajishauri!

Tumepiga kelele na tutaendelea kupiga kelele kuhusu hizi feeder roads,kwani zinatusaidia sana kukwepa misongamano ya magari ambayo inachosha na kusababisha upotevu wa masaa mengi ya kuzalisha.
Picha zinaonyesha barabara inayopitia Jangwani hadi kigogo,Mabibo na kutokezea Ubungo maziwa,lakini inavyoonekana pichani ni kipindi ambacho mvua hunyesha, ni dhughuli pevu kupita maeneo hayo.
Nafikiri TANROADS na wadau wote wanaliona hili, iwapo njia hii itatengenezwa kwa kiwango cha lami, nina uhakika hizi tunazoita foleni zitakuwa historia hapa Dar (Picha kutoka Blogu ya Michuzi).

Saturday, April 25, 2009

Kutoka MOI LEO!


Mustafa Mboweto(29) mkazi wa Goba amefikishwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili (MOI) leo baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu wa kushoto katika kifundo cha mguu (ankle joint).Amesema yeye alikuwa 'deiwaka' katika lori la mchanga ambapo lilifika njiano kukuta lori la kuuza maji likiwa limepaki kando ya barabara, wakati wakijiandaa kulipita lori hilo ghafla dereva aliliingiza barabarani.Kwa kuwa yeye na mwenzake walikuwa wameshuka ili kumuelekeza dereva wao jinsi kulipita lori hilo,dereva wa lori lao alipokuwa anakwepa aliwafuata na yeye kukanyagwa mguu.
Pichani ni Macdizel Kwimba(28) ambaye pia alifikishwa MOI baada ya mashine kumkatakata mkono na hatimaye mkono ukakatwa baada ya kuwa katika hali mbaya sana. Anasema anafanya kiwanda cha COTEX Mbezi Beach. Anasema alipokuwa akiendesha mashine ndipo mkono ukavutwa na 'kutafunwa' na mashine. Jana alipokelewa mgonjwa mwingine kutoka COTEX,Habiba Abdallah(29)mkazi wa Kunduchi Mtongani, ambaye alikatwa vidole na feni ya machine.Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa MOI amethibitisha kuwapokea majeruhi hao na amesema kwamba mara kwa mara wamekuwa wakipokea majeruhi wa kutoka COTEX wakiwa wameumia au kukatika mikono.
Wakati huo huo, Afisa Uhusiano wa MOI ametoa taarifa kwamba, Mkufunzi wa Chuo cha Zima Moto na Uokoaji, Bwana Marwa Mashana(37) amepokelewa hospitali hapo baada ya kupata ajali akiwa anaelekea Sokoine Morogoro. kufuatia ajali hiyo, ameumia mgongo(uliosababisha asiweze kuhisi kuanzia kiunoni hadi miguuni),mkono na kichwa.
wengine waliopokelewa leo ni Kulwa Hamisi(33)ambaye ameumia kichwa baada ya kugongwa na gari akiwa mtembea kwa miguu. E7758 PC Charles Emmanuel(36) mkazi wa Mtoni kijichi ambaye amevunjika mguu sehemu ya paja baada ya kupata ajali akiwa abiria wa Bajaji. Juma Musa(adult) wa kutoka Kibada, naye amepokelewa MOI akiwa amevunjika mguu sehemu ya paja, amegongwa na gari akiwa mtembea kwa miguu.
Kwa Mujibu wa Jumaa, wote wanaendelea vema.

Mbunge Afariki Katika Ajali!

                                                                  Mh. Phares Kabuye(MP)
Mbunge wa Biharamulo kwa chama cha TLP Phares Kabuye pamoja na watu wengine wawili wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magubike wilayani Kilosa jana saa 1 asubuhi.
Gari lililopata ajali lina namba za usajili T 934 ADA la kampuni ya RS Investment kama
linavyoonekana pichani.Lilikuwa likitoka Bukoba kuelekea Dar es salaam.
Inasemekana kwamba dereva wa basi alimpa "deiwaka" kondakta wake ambapo lilimshinda na kuacha njia akiwa katika mwendo wa kasi na hatimaye kupinduka. Kondakta na dereva wake hawajulikani walipo baada ya kukimbia (Picha:Bunge na Habari Leo na Bunge).
yES! Kilio changu kipo pale pale, tuungane kutokomeza jinamizi la ajali.

Friday, April 24, 2009

Ujumbe Kwa TANROADS!Big Up!

Pichani ni barabara iliyotengenezwa kwa kiwango cha lami hivi karibuni inayotokea Magomeni Mwembe Chai kwa Sheikh Yahya Jirani na Mwembechai Petrol Station. Sasa hivi barabara hii imepunguza sana msongamano,jitihada hizi zikifanyika kwa kutengeneza 'feeder roads' nyingine, itasaidia sana kuondoa msongamano.Ni matumaini yangu TANRODS wanaliona hilo!

Ujumbe Kwa TANROADS! Eneo Korofi!

Katika jitihada za kuhakikisha feeder roads zinafanyiwa matengenezo na kutumiwa na madereva ili kupunguza ajali,nimekuwa nikizifuatilia na kuzitumia hizi feeder roads mbalimbali. Kuna hii ya kutokea OilCom mwembechai kupitia Grand Hotel, DDC Magomeni Kondoa hadi Kawawa Road, narudia tena kwamba hii ni barabara muhimu kama itafanyiwa matengenezo. Kuna eneo korofi lililopo mbele ya DDC MAgomeni Kondoa ambalo majiu hutama mwaka mzima(Pichani).Mvua ikinyesha linakuwa dimbwi kubwa sana ambalo si rahisi kwa magari madogo kupita. Wahusika watuambie, kuna mipango gani!

Kutoka MOI!Shattered Dreams?


Kijana Salum Saleh baada ya kukatwa miguu yote
Kijana Salum Saleh(19) amelazwa taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili (MOI) kufuatia kupata ajali mbaya iliyosababisha yeye kupoteza miguu yote miwili baada ya madaktari kuona uwepo wake unahatarisha maisha ya Salum.
Anasema kwamba,yeye ni mchuuzi wa nguo mikononi, na siku hiyo alipanda daladala ili kutoka Mwenge kwenda Tazara. Dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha mwendo kasi na abiria wakaanza kumfokea ili apunguze. Yeye alikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wanakemea mwendo wa dereva huyo na alimfuata na kumwambia.Hii ilileta mtafaruku kidogo na ndipo wakati anashuka makondata walimsukuma, gari likampanda miguuni na kumsukumia katika mfereji wa maji machafu kiasi cha kumpa infection ambayo baada ya masaa machache miguu ilibadilika rangi na kuanza kutoa harufu mbaya sana.
Ili kuokoa maisha yake, ilionekana ni vema miguu yote iondolewe. Kijana Salum(pichana)amepoteza miguu yote,imebaki sehemu ndogo tu ya paja. Salum amekuwa mlemavu ghafla, ndoto za maisha yake zimeisha badilika na anakata tamaa ya kuishi.

(Salum Saleh,19,lost both legs following motor traffic accident. He was pushed by the bus conductor of a passenger bus he was in, following a misunderstanding between him and the bus operators. Having fallen down the bus tyres ran over his legs and pushed him in a drainage with contaminated water.His open wounds were infected instantly, which led to severe gangrene. Then,both limbs had to be amputated up to his thighs to save his life. Salum is desparate, lost hope and his life dreams are gone! )

Baada ya kupoteza Mkono!

Yasin amepoteza mkono wa kulia na baadhi ya vidole vya mkono wa kushoto
Yasin akielezea mkasa jitihada zake za kupata mkono bandia.

Yasin Ali(43) anasema anapata shida sana katika jitihada zake za kupata mkono wa bandia baada ya kupoteza mkono wake katika ajali iliyotokea mwaka 2003. Anasema kwamba, ajali ilimwacha akiwa hana mkono wa kulia na baadhi ya vidole vya mkono wa kushoto pia vilikatika.
Anasema amejitahidi sana kupata mkono bandia lakini jitihada zake zimegonga mwamba kwa sababu gharama ndio kikwazo kikubwa. mkono huo unauzwa Sh. 1,600,000 kufuatana na profoma invoive aliyokuwa nayo kutoka KCMC Moshi.
Yasin ameanza jitihada za kuwatafuta wasamaria wema ili waweze kumchangia aweze kutapata mkono huo. Kama umeguswa na utahitaji kumsaidia Yasin, tafadhali wasiliana nami nitakupa mwongozo wa jinsi ya kumpata.
(Yasin Ali,43, lost his right arm and some few fingers of  his right arm following motors traffic accident in 2003. To date he is stuggling to raise Tanzanian shilling 1.6million which is about 1500 US dollars for an artificial arm,but in vain)

Thursday, April 23, 2009

SUMATRA NA SEAT BELTS!

Ni hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) ilitoa tamko la kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha kwamba vyombo vyao vinakuwa na mikanda ya abiria(seat belts),lakini kinachoonekana ni kwamba wananchi pia hawajapata elimu ya kutosha juu ya matumizi na umuhimu wa mikanda hiyo. Hivi karibuni nilisafiri kwa basi la kampuni ya Scandinavia lenye namba za usajili T540 AGE,ambalo tayari lina mikanda hiyo lakini hakuna hata abiria mmoja aliyekuwa amefunga mkanda.Inaonekana dhahiri kwamba abiria waliokuwamo katika basi hilo hawajui hata matumizi ya mikanda hiyo.Nafikiri kinachotakiwa kwanza ni kuwatayarisha wananchi wafahamu umuhimu na kuwakumbusha mara kwa mara. Nchini Kenya wao walianzisha kampeni kama hiyo na wananchi walikuwa nafunga mikanda pale tu ilipotangazwa kwamba abiria atakayekiuka agizo hilo atatozwa faini na mwenye basi kufungiwa leseni ndipo waliona umuhimu wa kufunga mikanda na kikosi cha usalama barabarani kilikuwa kinasimamamisha magari na kukagua ili kuona ni nani hajafunga mkanda.Nafikiri kinachotakiwa kutangulia ni uhamasishaji na elimu ya kutosha ndipo adhabu kwa kukiuka agizo zianze kuetekelezwa.
Wananchi wanatakiwa kutambua ni kwanini wanahimizwa kufunga mikanda, na nina imani kwamba wakitambua hilo, hakutakuwa na haja ya kutumia nguvu ya ziada.Pia soma habari hii; http://ajali-traumaclass.blogspot.com/2009/03/mikanda-ni-muhimu-kwenye-mabasi.html
Abiria wakiwa wametulia raha mustarehe bila kufunga mikanda.
Mshale katika picha unaonyesha kifungio (buckle) cha mkanda kikining'inia chini bila kufungwa.
Abiria akiwa hana wasiwasi, mkanda unaning'inia pembeni kama mshale unavyoonyesha.

Udereva Huu? Mhhh!!

Picha hizi zinaonyesha magari yakikutana uso kwa uso katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi(bofya picha kuona vizuri). Nimeshuhudia madereva wakikosanakosana mara nyingi kwa sababu kila mtu anajiona ana haki ya  njia ya ziada. Wadau mnasemaje kuhusu hili?

Wizi wa Mifuniko ya Mashimo ya Maji Machafu!

Sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam na baadhi ya mikoa kama Tanga imekumba na wimbi la wizi wa mifuniko ya mashimo ya maji mchafu jambo ambali ni tishio kwa watembea kwa miguu na hata magari kama inavyoonekana pichani.
Baadhi ya magari yameharibika vibay baada ya kuingia katika mashimo hayo, na mengine yamegonga hata watu baada ya kuingia katika mashimo na kupoteza mwelekeo.
Inasemekana kwamba, mifuniko hiyo imeuzwa kwa wanaofanya biashara ya vyuma chakavu, na wengine wanasema kwamba huwa inauzwa kwa wajenzi wapya(photo from internet).

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker